Karibu kupakua vitabu vya bure kwa ajili ya kujiongezea maarifa na kukuwa kiroho.
HISTORIA YA KARISMATIKI KATOLIKI
Mkondo wa Karismatiki KatolilĀ«i ulianza mwaka 1967, yaani miaka miwili tu baada ya kufungwa kwa Mtanguzo Mkuu wa Piti wa Vatikani. Kwa miaka minane tu mfumo huo ulienea upesi mno na kutapakaa karibu nchi zote ulimwenguni. Katika kuenea huko, kuna ushahidi mahttsusi kwamba ulitapakaa wenyewe ukianzishwa katika nchi mbali mbali bila kuratibishwa, kupangiliwa au kuhamasishwa na vikundi vilivyokwisha….. Pakua kitabu kuendelea kujisomea
KARISMATIKI KATOLIKIĀ ILIVYOANZAĀ
Karismatiki ni mkondo wa namna gani, na imeanzaje ? Ni nani aliyeanzisha ?Ā Katika kurasa zifuatazo Mama Patti Gallagher Mansfield, ambaye ni kiongozi katika Karismatiki anayejulikana katika nchi mbalimbali na ni mama wa watoto wanne, anatupatia majibu ya msingi anapoeleza kwa njia inayogusa moyo ile asili ya Mungu kujitia kati, yaani tendo lile la enzi la Mungu lililo shina la Karismatiki Katoliki iliyopo duniani kote siku hizi. Anajua anaongea juu ya nini, kwa sababu alikuwa shahidi wa kwanza wa tukio lote lile.
Wakarismatiki hawana budi kufahamu vizuri mwanzo wa mkondo ambao wanakiri kwamba wamo. Lakini pia wale ambao hawamo, kwanza kabisa maaskofu, halafu mapadre, watawa na makatekista, watapata katika kurasa zinazofuata ufunguo wa kufahamu kazi ya ndani ya mkondo huo.… Pakua kitabu kuendelea kujisomea
KUTOKA UZINIFU HADI KUFIKIA UTAKATIFUĀ
āWaandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. Wakamwambia, āMwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hiiĀ ; nawe wasemajeĀ ?ā Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Wao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, āYeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe.ā Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho waoĀ ; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. Yesu akajiiunua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, āMwanamke, wako wapi wale washitaki wakoĀ ? Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatiaĀ ?ā Akamwambia, āHakuna, Bwana.ā Yesu akamwambia, ā… Pakua kitabu kuendeleaĀ kujisomea
Ā UKUAJI WA KIROHOĀ
Hali yetu kiroho inahitaji kukua. Hali hiyo ya kiroho ndio Ufalme wa Mungu ndani mwetu, ambao machoni pa watu ni kitu kidogo sana kisichoonekana kwa urahisi. Kwa wengi huonekana tu baada ya kumaliza shughuli za kawaida za kidunia. Kwa macho ya kawaida Ufalme wa Mungu ni mdogo sana, na watu hawana muda kwa mambo madogo. Ufalme huo kwa mtazamo mwingine ni kitu kinachokua, na uwezo wake wa kukua ni mkubwa sana, nao hukua na kuwa mkubwa kuliko matarajio ya watu. Nidyo maana Yesu alisema :
“Utawala wa Mbinguni umefanana na mbegu ya haradali ā¦ yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikioteshwa huwa kubwa kuliko mimea yote, hata ikawa mti” Mt. 13:31-32.
Tuangalie kwa pamoja kukua kwa huu utawala wa Mungu ndani mwetu, tukiufananisha pia na safari, hasa safari maalumu waliosafiri Waisraeli kutoka Misri Utumwani kwenda Kanaani nchi ya Ahadi. Tutaona Utumwa wa kiroho, jangwa la kiroho na nchi tuliyoahidiwa kiroho.
Jinsi safari ya Waisraeli ilivyokuwa ya ajabu na ngumu, ndivyo ilivyo safari ya kiroho. Njiani vizuizi na vipingamizi ni vingi kama ilivyokuwa kwa Waisraeli kule jangwani. Watakaoshikamana na Bwana mpaka mwisho ndio watakaoingia katika nchi ya Ahadi ambayo ni muungamo kamili na Mungu..… Pakua kitabu kuendeleaĀ kujisomea
MAISHA YAĀ WATAKATIFU MAKARI
Jina la Makari ni jina maarufu katika historia ya watawa walioishi jangwani mwa Misri. Tunamkuta mmoja aliyekuwa mfuasi wa Mt. Antoni na aliyemhudumia miaka kumi na mitano katika uzee wake. Huyu alikuwa mmojawapo aliyemzika Mt. Antoni. Mwingine alikuwa Mt. Isaka wa Fayoun aliyeambiwa na Bikira Maria kwenda kumwona Baba Antoni kupata baraka zake kabla hajaenda kwa njia ya mababa. Baada ya Mt. Antoni kufariki Makari huyu alishika nafasi yake ya kuwaongoza watawa.
Lakini miongoni mwa wakaa pweke katika nchi ya Misri wawili wamesifiwa sana kuliko wenzao walioitwa kwa jina hilo. Wote wawili walikuwa mashujaa wa Yesu Kristo wasioshindwa. Wote wawili walipadirishwa. Na wote wawili waliishi wakati wa Mt. Antoni, pengine walikuwa wafuasi wake. Hapa hatuna uhakika wa kutosha.
Mmoja wao, aliyetangulia kuzaliwa, alikaa karibu ya mji wa Theba, upande wa Kusini ya Misri. Alikuwa na fadhila bora na mwenendo wake ulikuwa wa ajabu kweli. Makari huyu huitwa mara nyingine Makari mkubwa kwa sababu alimtangulia mwenzake kuzaliwa au huitwa Makari Mmisri..… Pakua kitabu kuendeleaĀ kujisomea